BREAKING: Mahakama nchini Iran imetangaza kuwa imewatekelezea hukumu ya kifo wanaume wawili waliopatikana na hatia ya makosa yanayohusiana na maandamano makubwa yaliyotikisa nchi hiyo mwezi Januari mwaka huu. Kwa mujibu wa tovuti ya Mahakama ya Mizan Online , hukumu ya kunyongwa dhidi ya Abolfazl Sepahi na Amir-Hossein Safari ilitekelezwa Jumanne asubuhi. Shirika la habari la Mehr limeripoti kuwa adhabu hiyo ilitekelezwa hadharani katika uwanja mmoja wa mji wa Malekshahr , mkoani Isfahan , mbele ya wananchi. Mahakama imesema wawili hao walitiwa hatiani kwa madai ya kuwashambulia maafisa wa polisi kwa kutumia mapanga na visu, kuwafunga kwenye alama za barabarani, kuwaburuta, kuwamwagia petroli na kuwachoma moto wakati wa maandamano yaliyotokea Januari 8. Mbali na makosa hayo, walikabiliwa pia na mashtaka ya "moharebeh" (kupigana vita dhidi ya Mungu kwa kutumia silaha) pamoja na kosa la "kueneza ufisadi duniani" , wakidaiwa kuvuruga usalama na utulivu wa tai...